Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaj Batenga ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano muda wote utakapo hitajika kwa benki ya CRDB kwani benki hiyo imekuwa mdau muhimu wa maendeleo kwani wameendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungani wa Tanzania.
Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 6 Novemba 2024 ofisini kwake alipotembelewa na wadau kutoka benki ya CRDB kanda ya nyanda za juu kwaajili ya mazungumzo ili kuendelea kukuza na kuboresha huduma zao.
Aidha Mhe Batenga ametoa pongezi kwa benki ya CRDB kwa kuwa na huduma ya kibenki inayotembea (bank mobile service) hususani kwa maeneo ambayo hakuna matawi ya benki hiyo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wanaowahudumia katika maeneo yao wanayoishi au maeneo wanayofanyia kazi.
“Niwapongeze kwa kuwa na huduma inayotembea (mobile service) ambayo inasaidia sana kwa wakulima wetu huhssani kwa maeneo kama lupa na wakati mwingine ni vyema mkafanya utafiti wenu kuona uwezekano wa kufungua tawi Lupa ili kuwapunguzia adha wateja wenu kusafiri umbali mrefu kufwata huduma lakini pia kwa usalama wa fedha za wateja wenu”amesema Mhe.Batenga
Naye Meneja wa Biashara benki ya CRDB kanda ya ya nyanda za juu Bi Domina Mwita amesema kuwa lengo la ziara yao ni kutoa shukrani kwa Uongozi wa Wilaya ya Chunya kwa ushirikiano ambao wameendelea kuutoa kwao kamawadau wa benki hiyo lakini pia kufahamiana na kuona namna ya kuongeza wigo Zaidi wa kuwahudumia wanachunya katika Nyanja tofauti tofauti.
Bi Domina pia amekiri kupokea maoni yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya na kuahidi kuyafanyika kazi ili kuendelea kuboresha Zaidi huduma zao ikiwa ni pamoja na kuona namna ya kuwasaidia mikopo wachimbaji wadogo ili kukuza mitaji yao lakini pia kuendelea kutoa elimu za kifedha kwa wadau wao ili kukuza uelewa .
Wafanyakazi wa benki ya CRDB wametembelea ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kukutana na viongozi wengine na wadau mbalimbali wa Chunya na kufanya nao mazungumzo ili kuboresha na kukuza huduma zao pamoja na kuzichukua changamoto mbalimbali zinazowakumba wateja wao ili kufanya maboresho .
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaj Batenga akizungumza na wadau kutoka benki ya CRDB kanda ya nyanda za juu walipomtembelea ofisini kwake kuona namna kukuza na kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa Chunya.
Meneja wa biashara benki ya CRDB kanda ya nyanda za juu Bi Domina Mwita akielezea namna ambavyo wamejipanga kuboresha na kukuza huduma zao kwa wananchi wa Wilaya ya Chunya wakati alipokuwa akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Ofisini kwake.
Wafanya kazi wa Benki ya CRDB wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya wakati walipoketi ofisini kwake kwaajili ya mazungumzo juu ya huduma zao zinazotolewa na namna ya kuendelea kukuza huduma zao.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbaraka Alhaj Batenga wa pili kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB kanda ya nyanda za juu baada ya kumaliza mazungumzo yao .
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.