Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya anakumbusha wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kuzingatia muda wa Kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa Vijiji na vitongozi kwaajili ya Uchaguzi unaotaraji kufanyika November 27, 2024.
Taarifa mbalimbali kuhusu Uchaguzi huo zitaendelea kutolewa kupitia mitandao yetu ya kijamii na unapoona shaka yoyote usisite kuuliza. Wanachunya tujitokeze kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kupata viongozi watakao ongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, Hatima njema ya Chunya iko katika maamuzi yako kuchiriki, hivyo shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Endelea kufuatilia mitandao yetu na vyombo vya habari kwa ujumla
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.